airtel

airtel

.

.

Saturday, October 3, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA SHULE YA SEKONDARI YA J.K.NYERERE HUKO TARIME

MAMA SALMA KIKWETE APOKELEWA TARIME

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Capt. Mstaafu  Aseri Msangi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kwa ziara ya siku mbili mkoani humo tarehe 2.10.2015. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara.
 Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya utamaduni na wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga kilichoko katika wilaya yaTarime kwa ajili ya kuzindua rasmi Shule ya Sekondari ya J. K. Nyerere iliyojengwa na Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa North Mara Gold Mine
 Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya utamaduni na wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga kilichoko katika wilaya yaTarime kwa ajili ya kuzindua rasmi Shule ya Sekondari ya J. K. Nyerere iliyojengwa na Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa North Mara Gold Mine
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu Glorius Luoga muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Nyamwaga kwa ajili ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari J K Nyerere.
 Mama Salma Kikwete akijumuika na viongozi wa Mkoa wa Mara na wanachi wa Kijiji cha Myamwaga kusherehekea uzinduzi rasmi wa Shule ya J.K. Nyerere iliyojengwa na North Mara Gold Mine.
 Mama Salma Kikwete akitoa hotua ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari J.K.Nyerere katika Kijiji cha Myamwaga kilichoko Mkoani Mara.
 Mama Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa Mkoa wa Mara na wale wa Wilaya ya Tarime na wahisani waliojenga Shule ya J.K. Nyerere kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Shule hiyo iliyoko katika Kijiji cha Nyamwaga.
 Mama Salma Kikwete baada ya kukata utepe hapa anakiondoa kitambaa kukamilisha sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza Ndugu Jimmy Ijumba, Meneja wa ACACIA –North Mara Gold Mine mara baada ya kuzindua rasmi shule hiyo 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga ikiwa ni ishara ya kuagana nao baada ya kuifungua rasmi Shule ya Sekondari J.K. Nyerere iliyoko katka Wilaya ya Tarime.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...