VANESSA MDEE NA JUX WAAHIDI KWA MASHABIKI WAO KAZI NZURI YA PAMOJA
MKALI
wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V Money’ na Juma Jux ‘Jux’,
wamesema baada ya kila mmoja kukamilisha kazi zake ndipo watatoa nyimbo
zao za ushirikiano ambazo wamesharekodi. Aliongeza kwamba, kutokana na
kila mmoja kuwa na kazi zake nyingi, hawataweza kufanya kazi ya pamoja
hadi kila mmoja atakapomaliza, maana wazo hilo walikuwa nalo muda mrefu
na wameshalifanyia kazi, ingawa hawataki kuzitoa kwa sasa. “Tumeshafanya
nyimbo za pamoja nyingi, lakini hatutatoa kwa sasa kutokana na kuwa na
kolabo na wasanii wengi, naye kuwa na kazi zake hivyo kila mtu akimaliza
‘project’ zake ndipo tutatoa nyimbo zetu za ushirikiano,’’ alisema V
Money.
No comments:
Post a Comment