Katika siku kadhaa zilizopita kumekuwa na
matangazo kadhaa hasa kwenye mitandao ya kijamii juu ya simu mpya
inayouzwa kwa ushirikiano wa makampuni mawili nguli ya mawasilino
nchini. Huawei ambao ni watengenezaji wa simu kwa ushirikiano na Tigo.
Baadhi ya watu maarufu wamekua
wakiizungumzia kwenye kurasa zao binafsi. Kama unavyooa Dina Maris hapo
juu. Kama mtandao wa masuala ya teknolojia, nikaona si mbaya kama
tutaitazama simu husika, ili kujua kama YALIYOMO YAMO.
Simu hii inauzwa shilingi 160,000 kwenye
maduka ya Tigo ambapo utarudishiwa pesa uliyonunulia kama vifurushi kwa
miezi sita. Hii ni ofa nzuri kwa simu yenye sifa hizi.
Simu hii inatumia Android OS, v4.4.4
(KitKat), kioo cha inchi nne na CPU Quad-core 1.2 GHz Cortex-A7. Ina
Camera mbili, ya mbele (maalumu kwa SELFIE) ina 2MP na ya nyuma ina 5
MP, 2592 х 1944 pixels, flash mbili.
Waswahili husema kizuri hakikosi kasoro,
Je kuna kasoro gani nilizoona kwenye simu hii? Ukweli ni kwamba sikuona
tatizo lolote. Bei yake ni ndogo sana ukifananisha na sifa za simu hii.
Kama unahitaji simu bora kwa gharama nafuu basi hii ni simu kwa ajili
yako.
No comments:
Post a Comment