airtel

airtel

.

.

Wednesday, January 6, 2016

HAPA KAZI TU MWALIMU MKUU ALIYEKAIDI AGIZO NA KUCHANGISHA MICHANGO ACHUKULIWA HATUA MWANZA


OFISA Elimu Mkoa wa Mwanza (REO), Hamis Maulid, amesema Serikali imemvua madaraka mwalimu mkuu mmoja kwa kukaidi agizo la kufuta michango na ada lililotolewa na Rais John Pombe Magufuli na imeahidi kuwachukulia hatua walimu wakuu na watendaji wote watakaoshindwa kutimiza wajibu wao.

Alisema, Serikali haitakuwa na mchezo wala huruma kwa walimu wakuu watakaokaidi agizo lake la kufuta ada na michango yote kwa shule kuanzia awali hadi kidato cha nne mwakani.

Maulid alitoa kauli hiyo jijini hapa juzi, wakati akizungumza katika kikao kazi cha utekelezaji wa Waraka wa Elimu Namba 6 uliotolewa na Serikali, ambacho kiliwahusisha Walimu Wakuu wa shule za msingi na sekondari, Watendaji wa Kata na Mitaa, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wataalamu wa Idara ya Elimu.Alisema kuwa, Serikali itatoa fedha wa uendeshaji wa shule, hivyo hakutakuwa na michango na watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua.

"Bahati nzuri serikali imefuta ada na michango yote imeondolewa, hilo si ombi ni agizo.Wapo watakaokaidi na tayari mwalimu mkuu mmoja wa shule tumemvua madaraka. Hilo hatutakuwa na mchezo wala huruma na tumeanza kuchukua hatua kwa wakuu wa aina hiyo," alisema Maulid.
Alisema, Maofisa Elimu wasikae maofisini, waende shuleni wakae na kuzungumza na walimu ili kero zao zipungue ingawa inawezekana zisiishe,lakini pia madai yao halali walipwe.

"Tunataka watoto wasome tupate wataalamu na tunataka kero za walimu zipungue,inawezekana zisiishe.Yafanyike majaribio kwa kushindanisha shule kwa ngazi ya kata na kata, wilaya kwa wilaya na mengine yatakayofaa ili kuboresha kiwango cha elimu," alisema.

Alisema licha ya Mkoa wa Mwanza kushika nafasi ya tatu kitaifa kwenye mitihani ya kuhitimu darasa la saba, Wilaya ya Nyamagana kati ya halmashauri 166 imeporomoka baada ya kushika nafasi ya 40 kitaifa kutoka nafasi ya 22 mwaka jana.

Alisema kuwa wanafunzi 42,142 sawa na asilimia 82.2 ya watahiniwa 51,312 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, huku Wilaya ya Ukerewe ikifanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa na ya 5 kitaifa ya pili ni Ilemela na ya 10 kitaifa kutoka 30 mwaka jana na kuzitaja shule 10 bora kuwa ni Mugini, Alliance,St.Kalori na Chapamba ambayo ni ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...