airtel

airtel

.

.

Wednesday, January 9, 2013

KITALE: AROBAINI YA SHAROMILIONEA WASANII WALIOTOA MCHANGO NI WATANO TU


MWIGIZAJI wa filamu na Komedi Mussa Yusuf ‘Kitale’ amaewashukia wasanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya Bongo fleva kwa kusema ni wanafiki hawana urafiki wa ukweli kati yao msanii huyo alisema hayo kufuatia kuzorota kwa arobaini ya rafiki yake kipenzi marehemu Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’ kuhudhuriwa na wasanii wachache na kuchangiwa na watu watano tu. “Nimejifunza mengi kutoka kwa watu na nimewajua rafiki wa kweli lakini wengi ni wanafiki walikuwa wanajifanya Sharo rafiki yao kumbe hakuna lolote, kwa mfano tulipanga shughuli ya Arobaini ifanywe na sisi wenye siyo Bi. Mkubwa lakini waliochanga ni watu watano tu, kuna ushikaji kweli hapa’? anasema Kitale.

Kitale anasema kuwa Sharo alikuwa na marafiki wengi ambao walikuwa hawakauki kwake lakini katika msiba hawakudhuria akiongelea kuhusu Bongo Movie alisema anamshukru sana Mtunis ambaye alijitoa sana katika msiba toka mwanzo hadi mwisho na Kitale anaomba Mtunis awe kaka yake wa karibu akiamini kuwa ni rafiki wa kweli, Kitale katika kumaliza machungu yake ametunga wimbo maalum kwa Sharo ambao utawachana Bongo Movie na Bongo Fleva.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...