airtel

airtel

.

.

Wednesday, January 9, 2013

MAANA RAHISI YA KING'AMUZI

http://sattvng.files.wordpress.com/2010/08/startimes-decoder7.jpg
Stesheni zote za TV zina mitambo yake ya kurushia matangazo mfano,TBC,ITV,RFA n.k zote kila moja ina mitambo yake,na mikoani wana busta zinazorusha matangazo.
  Mitambo hiyo huweza kurusha matangazo na yakapokelewa na Antena za kawaida za kupokea na kurusha matangazo katika TV.
Mitambo hiyo huweza kurusha matangazo kwa maeneo maalum tu,mitambo hiyo ndiyo inayoitwa ANALOJIA au mitambo ya analojia.
Suala la Dijitali ni stesheni hizo za TV,zinarusha matangazo yake moja kwa moja katika mitambo inayopeleka moja kwa moja kwenye satelaiti ambapo matangazo hayo huweza kuonekana Dunia nzima.
kwa yule mwenye tv anayetaka kuona matangazo hayo inabidi awe na dikoda au king'amuzi ambacho ndicho kitamuwezesha Tv yake kuonyesha matangazo ya stesheni mbalimbali kwa mujibu wa programu iliyowekwa katika king'amuzi hicho kwa idadi ya stesheni za kuangalia kutegemeana na kiasi cha malipo yaliyopangwa. zipo stesheni ambazo ni za bure zisizolipiwa.
Kwa vile Teknolojia ni suala la kimataifa na maamuzi yake hutolewa na Mashirika mbalimbali makubwa ya kimataifa,suala la kuzimwa kwa mitambo ya Analojia na kuanza kutumika kwa mitambo ya Dijitali tu,ni suala la kimataifa,SISI HATUNA MAAMUZI NALO BALI NI WATEKELEZAJI.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...