JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha
wananchi na wadau wengine kuwa hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt.
Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 saa 6:00 mchana katika Viwanja
vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi
wa Serikali, Vyama vya Siasa, Taasisi za kidini, Asasi za kiraia na wananchi wa
kawaida.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba
anatarajia kuwakabidhi Waheshimiwa Marais, ripoti ya mchakato wa Katiba na
rasimu ya Katiba.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya
wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia
mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, anuani za posta, tovuti (www.katiba.go.tz)
na ukurasa wa facebook wa Tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).
Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko
ya Katiba,
Dar es Salaam
Disemba 27, 2013.
No comments:
Post a Comment