Baadhi ya mashabiki wa ligi ya bata wakifuatilia mojawapo yamapambano. |
Baadhi ya wachezaji wakicheza soka. |
Hapa ni ‘wanaume kazini’ |
Mwasisi wa ligi ya bata, Hussein Abdul akipozi kwa kamera |
(NA GABRIEL NG’OSHA/GPL)
Stori:Na GABRIEL NG’OSHA
KIJANA Hussein Abdul (19) wa Magomeni-Makanya jijini
Dar, ameanzisha ligi ya soka kwa vijana wa eneo hilo ambapo mshindi
miongoni mwa timu shiriki nane, atatwaa bata (ndege) wawili na mfungaji
bora atazawadiwa sh. 4,000.Hussein ambaye ni mpenzi mkubwa wa soka na ambaye huandaa ligi hiyo kila shule zinapofungwa, ametoa wito kwa wafadhili kusaidia juhudi zake kwa kuwapatia vifaa vya mchezo huo kama vile viatu, jezi, mipira, vipenga, magoli, ukarabati wa kiwanja na mafunzo.
Amesema atakayekuwa tayari kusaidia juhudi zake ampigie simu kwa namba 0654595064 ambayo imesajiliwa kwa jina la Aziz Ally.
No comments:
Post a Comment