airtel

airtel

.

.

Wednesday, December 20, 2017

TUME MPYA YAUNDWA KUCHUNGUZA MALI ZA CCM NCHI NZIMA

Taarifa iliyotolewa December 20 2017 kuhusu yaliyojiri katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kikao cha kwanza baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Tisa wa Mwaka 2017 imeeleza kuwa Rais Magufuli ameunda Tume ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakayokuwa na jukumu la kwenda kufuatilia Mali za Chama kote nchini Tanzania.
Wafuatao wameteuliwa kuwa katika Tume ya CCM ya kufuatilia na kuhakiki Mali za Chama; -
1. Dkt. Bashiru Ali Kakurwa – Mwenyekiti wa Tume
2. Walter Msigwa – Mjumbe
3. Albert Msando – Mjumbe
4. Galala Wabanhu (Hananasif) – Mjumbe
5. Albert Chalamila – Mjumbe
6. William Sarakikya – Mjumbe
7. Komanya Kitwara – Mjumbe
8. Dkt. Fenela Mkangara – Mjumbe
9. Mariam Mungula – Mjumbe
Tume hii itafuatilia mali za Chama kokote ziliko na itamhoji kila mtu anayehusika katika Chama na katika Serikali.

Sunday, July 2, 2017

GEITA KINARA WA MICHEZO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akimkabidhi kombe mwanafunzi ambaye amewakilisha mkoa wa Geita katika michezo hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba, mkoani Mwanza.

Saturday, July 1, 2017

FATNA RAMOLE MTANGAZAJI WA AZAMN TV HAJULIKANI ALIPO KAMA UMEMUONA POPOTE,SOMA HAPA

 Image may contain: 1 person


Una taarifa zozote kuhusu Fatna Ramole? @fatnaramole
Mfanyakazi mwenzetu @azamtvtz hajulikani alipo.
Unaweza kutoa taarifa zake kwa namba hii
0719669749
Asante. @ Dar es Salaam, Tanzania

MASTAA MBALIMBALI WA SOKA WAHUDHURIA NDOA YA LIONEL MESSI JUNE 30,2017

MESSI AVUNJA UKIMYA ACHUKUA JIKO RASMI








Usiku wa Ijumaa ya June 30 staa wa soka wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi alifunga ndoa na mpenzi wake wa toka utotoni Antonella Roccuzzo ambaye pia wamezaa nae watoto wawili wa kiume.













Messi na Antonella Roccuzzo walifahamiana toka Lionel Messi akiwa na umri wa miaka mitano na Antonella Roccuzzo ambaye ni mke wake kwa sasa akiwa na umri wa miaka 4, wameamua kufunga ndoa kwao Argentina ndoa ambayo ilihudhuriwa na wachezaji wenzake na marafiki zake mbalimbali.
Zaidi ya marafiki wa Lionel Messi wanaofikia 250 walisafiri kwa ndege binafsi kuelekea Argentina kuhudhuria harusi ya staa huyo ambayo simu za mkononi zilikuwa zimefungiwa kufanya kazi ndani ya ukumbi sherehe ilipo kwa lengo la kuweka privacy pamoja na ulinzi wa askari zaidi ya 450.


Rapper wa Marekani, Future amethibitisha show yake ya Tanzania, Julai 22.

TANZANIA YATAJWA KATIKA ZIARA YA MSANII WA MAREKANI FUTURE



future

Future ametoa orodha ya ziara yake ya muziki ya ‘The Future Hendrxx Tour’ na Tanzania ni moja ya nchi ambayo Tour hiyo itatembelea.
Future atatumbuiza Tanzania pamoja na Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na Weusi.

BEI MPYA ZA MAFUTA KUANZA LEO JULAI 1,2017






Ikiwa tunaanza mwezi julai leo, kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA ambao wametangaza kushuka kwa bei mpya za mafuta ya vyombo vya moyo ikiwemo magari na mashine. Bei hizi elekezi zimeanza kutumika rasmi leo July 1, 2017.
Nimekuwekea hapa chini bei za mafuta kwa nchi nzima kuanzia kesho Jumamosi July 1, 2017.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...